Enrolment options
MLS6142 Mofosintaksia ya Kiswahili
Semester 1
Moduli hii inahusu Mofosintaksia ya Kiswahili. Ni moduli inayozingatia vipengele mbalimbali vinavyohusiana na muundo wa Kiswahili kwa kuchunguza kwa pamoja viwango vya Mofolojia na Sintaksia ya Kiswahili. Ili kutalii maswala muhimu kuhusu Mofosintaksia ya Kiswahili, viwango vingine vya uchunguzi wa kiisimu vimeshughulikiwa kwa kiasi fulani katika moduli hii. Hivyo, mwanafunzi ataweza kunufaika kwa kuyachanganua maswala yenyewe ambapo mwingiliano kati ya vipashio vinavyounda lugha utaangaziwa. Pamoja na hayo, muundo wa Kiswahili utachunguzwa kwa kuzingatia nadharia za kisasa za uchunguzi wa kiisimu ambapo maswala ya ufundishaji na ujifunzaji wa muundo wa Kiswahili yatajadiliwa kwa kina.