Enrolment options

DTMSE13: Mbinu za Ufundishaji wa Kiswahili and English Teaching Methods (DTP)
Arts and Languages

Moduli hii inakusudia kuwawezesha wanafunzi kuwa na maarifa na ujuzi wa kufundisha somo la Kiswahili kama lugha ya pili kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini Rwanda.

Hivyo basi, historiografia ya ufundishaji wa lugha ya pili kuanzia karne ya 19 inapitiwa. Hii inafanyika ili kuwawezesha wanafunzi kuzifahamu vema mbinu mbalimbali za ufundishaji wa lugha ya pili. Kwa kufanya hivyo, wanafunzi kama walimu tarajali watakuwa katika nafasi ya kuweza kuzifahamu kwa ukamilifu mbinu zote za ufundishaji wa lugha ya pili na hivyo kufanya uamuzi sahihi wa mbinu ipi inayofaa kutumiwa kutokana na mazingira wanayokutana nayo.

Aidha, uhusiano baina ya mbinu, mkabala na ufundi  au uhusiano baina ya mbinu, mkabala usanifu au uundaji na utaratibu pia umepitiwa. Mambo mbalimbali ya msingi katika ufundishaji wa lugha ya mazingatiwa. Mambo haya ni kama vile aina mbalimbali za mtaala, zana na nyenzo za ufundishaji, maandalio ya somo, malengo ya elimu nchini Rwanda na Malengo ya ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili nchini Rwanda.

2024 Self enrollment
2024 Self enrollment