Enrolment options
SWA2142: Nathari Bunilizi na ushairi wa Kiswahili (DTP)
Arts and Languages
Moduli hii ina sehemu kuu mbili: nathari bunilizi kwa sehemu ya kwanza na ushairi katika sehemu ya pili. Sehemu ya kwanza inazamia kwa ukamilifu nathari bunilizi hsususani riwaya ya Kiswahili, hadithi fupi andishi za Kiswahili pamoja na novela. Historia ya maendeleo ya nathari hizi bunilizi zinashughulikiwa ikiwa ni pamoja na sifa zake bainifu pamoja na uhakiki wake. Sehemu ya pili inahusika na ushairi. Mjadala kuhusu fasili ya ushairi, sifa bainifu za ushairi, maendeleo ya ushairi pamoja na uhakiki wa ushairi ni miongoni mwa mambo muhimu katika sehemu hii. |